MWANDISHI WA HABARI ZA DAWA ZA KULEVYA AUWAWA MTAANI


Marehemu Javier Valdez

Watu wasiojulikana wamempiga risasi mwandishi maarufu wa habari za biashara ya dawa za kulevya wa Mexico, Javier Valdez. Mwandishi huyu amepigwa risasi katika mji wa  Culiacan ambako ndiko alikokuwa akiishi na kufanya kazi. Valdez amefariki akiwa na umri wa miaka 50. Mwaka 2011 alipata tuzo ya International Press Freedom Award iliyotolewa na Committee to Protect Journalists (CPJ), kutokana na kazi yake nzuri.  Valdez ameingia kwenye orodha ya waandishi kadhaa ambao wameuwawa nchini Mexico mwaka huu. Katika miaka 30 ya kazi yake ya uandishi Valdez aliandika mengi sana kuhusu biashara ya madawa ya kulevya na hata akaliongelea kundi baya sana la biashara hiyo Sinaloa Drug Caltel,inasemekana asilimia 25 ya dawa za kulevya zinazoingia Marekani kutoka Mexico zinaingizwa na kundi hili. Mwanzilishi wa kundi hili Joaquim Guzman maarufu kwa jina la El Chapo (Fupi) alikamatwa mwaka 2014 na anasubiri kesi yake huko Marekani. Mexico this year.

Valdez alipigwa risasi mtaani jirani kabisa na ofisi za gazeti lake la kila wiki alilokuwa akilimiliki.
Rais wa Mexico Enrique Peña Nieto amelaani mauwaji hayo.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.