PICHA ZA UTUPU ZA MGOMBEA URAIS, MTIHANI KWA MGOMBEA


Diane Shima Rwigara
YULE binti wa Kinyaruanda aliyetangaza nia ya kugombea Urais mwezi wa nane mwaka huu, kuingia katika kinyang’anyiro ambacho kingempambanisha na Rais wa sasa wa Rwanda Rais Paul Kagame, na pia kuwa mwanamke wa kwanza nchini humo kugombea nafasi hiyo, amekumbana na kizingizti kikubwa baada ya picha zinazodaiwa ni zake akiwa mtupu kusambaa katika mitandao ya kijamii kuanzia siku ya Ijumaa. Diane Shima Rwigara mwenye umri wa miaka 35, ambaye amekuwa mwanaharakati wa kudai uhuru wa kujieleza amekuwa kimya kabisa baada ya kusambaa kwa picha hizo. Ukurasa wake wa twitter haujabadilika toka May 2 na ukurasa wake wa Facebook haujabadilishwa kuanzia April 28.  Jumatano iliyopita, kabla ya kusambaa kwa picha hizo aliitisha mkutano wa vyombo vya habari na kusema, ‘Kila mtu anaogopa kujieleza, kwa kuwa wanaogopa sana chama tawala, nikiwa Rais nitashughulikia umasikini, haki kwa wote na usalama”. Toka picha hizo kumwagwa hadharani,  wanaomuunga mkono wamekuwa wakijaribu kumpa moyo kuwa picha hizo ni za kutengeneza hivyo asife moyo.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.