POLISI 11 WA KENYA WAUWA KWA MABOMU YA KUTEGWA KANDO YA BARABARA


Bomu lililotegwa kando ya barabara limeua polisi wawili nchini Kenya. Kuuwawa kwa polisi hawa kumefanya idadi ya wanausalama wa Kenya waliouwawa kwa mabomu yaliyotegwa kando ya barabara wiki hii kufikia 11. Milipuko hii ambayo inadaiwa ilitegwa na wapiganaji wa Al Shaabab, inaonyesha ugumu wa kazi waliyonayo wanausalama nchini Kenya katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo. Kuhusu tukio la kuuwawa kwa bomu , Kamishna wa polisi wa County ya Garissa James Kianda alisema askari wake walikuwa wanaenda kuongeza nguvu za ulinzi, kiasi cha saa nne usiku wakati gari lao lilipolipuliwa na bomu na kutegwa katika eneo la Liboi jirani na mpaka wa Kenya na Somalia, askari wawili walifariki na wawili walijeruhiwa. Kabla ya hapo Al shabaab walitangaza kuhusika na mabomu ya kutega yaliyowauwa askari wanane siku ya Jumatano. Al shabaab wanadai wanawashambulia askari na wananchi wa Kenya kwa kuwa nchi hiyo ilipeleka askari kupigana Somalia toka mwaka 2011. Askari wa Kenya ni kati ya askari 22,000 wa jeshi la kulinda amani linaloisaidia serikali halali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa kuweza kutekeleza majukumu yake.

Vurugu za Somalia zilianza mwaka 1991, ambapo serikali ya huko ilipinduliwa kisha makundi mbalimbali ya Kisomali yakaanza kupigana yenyewe kwa yenyewe

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.