RAIS MPYA WA UFARANSA ANA MIAKA 39 TU, MKEWE ANA MIAKA 64


RAIS MACRON NA MKEWE
Emmanuel Macron amekuwa Rais mpya wa Ufaransa. Macron ameshinda uchaguzi wa nchi hiyo baada ya kuzoa 66.06% ya kura zote na kumwangusha mpinzani wake Marine Le Pen na kuwa Rais kijana kuliko wote waliowahi kuongoza nchi hiyo. Macron ana umri wa miaka  39 tu. Jambo jingine kubwa ni kuwa Macron ni Rais wa kwanza kuchaguliwa kutoka nje ya vyama vikuu viwili vya siasa vya nchi hiyo toka mwaka 1958. Maisha yake binafsi ni hadithi nyingine kubwa tu. Mke wa macron anaitwa Brigitte Trogneux ana umri wa miaka 64, walioana mwaka 2007. Bibi huyu alikuwa mwalimu wa uigizaji wa Macron. Mama huyu alishawahi kuongea na gazeti moja na kuwaaambia kuwa Macron alipokuwa na miaka 17 alimwambia kuwa iwe isiwe lazima atamuoa. Uhusiano wao ulianza wakati Macron ana umri wa miaka 16 tu, kiasi cha wazazi wa mvulana huyu kumkanya bibi huyu amuache mtoto wao mpaka afikie japo umri wa miaka 18. Bibi huyu ndie mshauri mkuu wa Macron na hufwatilia kila kitu kinachoandikwa au kusemwa kuhusu mumewe na kutoa ushauri


No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.