RIPOTI YA USAFIRISHAJI WA MCHANGA WA MADINI INATISHA INASIKITISHA, WAZIRI MATATANI


Profesa Muhongo
Leo kamati iliyopewa kazi na Rais Dr John P Magufuli kufuatilia taratibu za usafirishaji wa mchanga wa madini(makinikia) imekabidhi taarifa yake kwa Rais, ripoti ambayo baada ya kusomwa imewaacha Watanzania wengi midomo wazi. Ripoti hiyo imeonyesha kuwa kwa miaka mingi, na hasa  kuanzia 1998 ambapo usafirishaji wa mchanga wa madini ulianza, serikali ya Tanzania imepoteza matrilioni ya fedha. Katika hali ambayo ni wazi ilikuwa inalenga kufanya ufisadi, takwimu zilizokuwa zikitolewa na wasafirishaji ni za uongo na serikali kwa upande wake ilikuwa haiweki taratibu zozote ambazo zingewezesha kufuatilia ukweli wa takwimu hizo. Swala la kusafirisha mchanga wa madini nje ya nchi, lilianza kupigiwa kelele muda mrefu na watu mbalimbali, na wengi waliulizwa kwanini kusianzishwe taratibu za kuyeyshusha mchanga huo hapahapa nchini? Visingizio vimekuwa vingi, kumekuweko na maelezo kuwa  gharama ya kuweka kiwanda cha aina hiyo nchini ni kubwa kuliko madini yanayopatikana na hata mara nyingine kisingizio cha swala la umeme kutajwa kuwa ni moja ya kikwazo cha kutokuwa na teknolojia hiyo, uwongo huo umetoa nafasi kwa mchanga kuwa unasafirishwa nje miaka yote hiyo.

Baada ya kusikiliza ripoti hiyo, Rais amemtaka waziri wa Nishati na Madini Profesa Muhongo kujitafakari kuhusu swala hili. Pia Rais amevunja

Bodi ya Tanzania Minerals Audit Agency (TMAA) na Rais ameagiza uchunguzi uanze kufanywa na vyombo vya usalama kuhusu uhusika wa watendaji wake katika sakata hili la usafirishaji wa kifisadi wa mchanga wa madini.  

 
Huu ni muhtasari wa kamati ya uchunguzi wa mchanga wa madini kama ulivyowasilishwa na mwenyekiti wake Prof Mruma hii keo Ikulu.HADIDU ZA REJEA!.1.Kamati ilikuwa na kazi ya kuchunguza aina na kiwango cha madini yaliyopo ndani ya mchanga wa madini unaosafirishwa nje!.2.Chimbuko la utafiti huo ni kutojulikana kwa kiwango cha makinikia na mikataba yake!.3. Hadidu za rejea zilikuwa ,Kufanya uchunguzi wa makinikia kwenye bandari ya dsm na migodini,Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kujua thamani na aina ya madini yaliyopo kwenye makilikia,kuchuza uwezo wa scanner zilizopo bandarini,kuchunguza uwezo wa TMAA katika kusimamia makinikia,4.Kamati ilitembelea bandari ya Dsm,bandari kavu na kwenye migodi ya Bulyanhuru na Buswagi,yapo makontena ambayo kamati ilichukua sampuli ya juu na chini,sampuli nyingine ilikuwa zigzaga!.5.Kamati ilichunguza uwezo wa scanner kupima makinikia!.6.Kamati ilikokotoa thamani ya madini yaliyopatikana kwenye makinikia!.MATOKEO YA UCHUNGUZI1.Kamati imebaini uwepo wa dhahabu kiasi Kikubwa cha dhahabu kwenye makinikia,katika makontena 277 yaliyozuiliwa kulikuwa na tani saba za dhahabu!.

2.Makontena 277 yaliyozuliwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi Trilioni moja nukta moja nne saba!.3.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya shaba,Silver,surpher,chuma.4.Copper pekee ilikuwa ya thamani ya shilingi Bilioni 23.3,hapa kulikuwa na tofauti kubwa na ripotibya serikali ambayo ilionesha kuwa na thamaninya Bilioni 13.4.Upande wa silver kamati ilibaini uwepo wa silver ya thamani ya bilioni 2.1.tofauti na ripoti ya Serikali ilionesha thamani ya Bilioni 1.5.Upande wa surpher kamati ilibaini uwepo wa surpher ya thamani ya shilingi bilioni 1.9,kamati ilibaini madini madini haya hayapo katika mrabaha6.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya chuma yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3,7.Kamati ilibaini uwepo wa madini mkakati ambayo kwa sasa yanahitajika sana duniani yenye thamani kati ya bilioni 129.5 mpaka  bilioni 261.5Thamani ya madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyochunguzwa kamati imebaini yana thamani ya triloni 1.339,ambazo serikali haipati hasa senti moja na hayapo kwenye mrabaha!.8.Kamati imegundua uwepo wa madini mengine mengii ambayo hayarekodiwi kwenye nyaraka za serikali!.9.Kamati imebaini wakala wa madini Tanzania hawafungi utepe kwenye makontena kuonesha viwango vya madini,kamati imebaini ufungwaji huu kufanyika wakati wa kusafirisha makontena.10.Kamati imebaini scanner za bandarini kutokuwa na uwepo wa kubaini utotoshwaji wa mali!.MAPENDEKEZO YA KAMATI1.Serikali isitishe usafirishaji wa mchanga nje ya nchi2.Serikali ihakikishe mitambo ya kusafisha makinikia unafanyika nchini3.TMAA ifunge utepe mara baada ya mchanga kupakiwa kwenye makontena!.4.TMAA ipime metal zote kwenye makininia5.TMAA ipime viwango vyote vya makinikia na madini kwenye mbar bila kujali ripoti ya msafirishaji hii itasaidia Serikali kupata mrabaha!.6.Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wizara husika.7.Serikali iweke mfumo kushtukiza kwenye udhibiti wa madini!.8.Serikali itumie wataalam wa mionzi kwenye scanner za bandarini!.

2 comments:

  1. Mungu ibariki Tanzania, japo hili jipu limetusuka

    ReplyDelete

Post Top Ad

Powered by Blogger.