SINEMA LA JACK PEMBA BADO BICHI KABISA


Kampala — Polisi wa jijini Kampala wamehakikisha kuwa wanamshikilia  Jack Pemba. Msemaji wa polisi jijini Kampala, Mr Emilian Kayima, amehakikisha kuwa Jack alikamatiwa kwenye uwanja wa ndege wa Entebbe International Airport kutokana maelekezo kutoka Mahakama Kuu ya Uganda kitengo cha biashara. Maelezo ni kuwa April 11, 2017 Steve Stavropolos aliyekuwa akimdai Jack Pemba, aliweza kupata warrant ya kumkamata Jack Pemba ambayo ilikuwa imetiwa sahihi na Msajili Mwandamizi wa Execution Division wa Mahakama hiyo, Mr Pemba alikuwa amehukumiwa na tamko lilikuwa limetolewa na mahakama likihusu kesi  No. 509 ya 2016, kuwa Jack amlipe mdai $756,257.9 pia liamriwa kulipa pesa ya Uganda Shs 31, 766, 272 kama gharama za kesi.  Arrest warrant hiyo ilikuwa imeandikwa hivi
"This is to command you to arrest the said debtor unless the said judgment debtor Jack Akim Pemba pays you the sum of $756,257.90 and Shs 31,766,272 together with... .for the cost of executing the arrest warrant to bring the said judgment debtor before court with convenient speed,"
Bwana  Kayima alisema kuwa polisi wamefanya kazi yao kwa umakini na kumtia nguvuni Jack Pemba wakati akitaka kuondoka nchini.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.