TRUMP ALITOA SIRI KWA URUSI?


Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi  Sergey Lavrov, Rais Donald Trump na Balozi wa Urusi Marekani Sergey Kislyak.
Shirika la utangazaji la CNN limekuja na tuhuma nzito sana. Kwa maelezo ya chombo hiki Rais Donald Trump alimueleza Waziri wa Nje wa Urusi mambo ambayo ni siri sana, Wamarekani huita siri hizi (highly classified information). Ukielewa kuwa mpinzani namba moja wa Marekani ni Urusi, uzito wa tuhuma hizi ni mkubwa sana. Tuhuma hizi zilitolewa hadharani kwa mara ya kwanza na gazeti la The Washington Post siku ya Jumatatu. Pamoja na Ikulu ya Marekani kutoa maelezo kadhaa kuhusu hilo na kisha mshauri mkuu wa Rais wa mambo ya Usalama H. R McMaster  ambaye nae alishiriki katika mikutano ambayo inadaiwa Trump alitoa siri hizo, alimtetea Rais wake na kusema hakuna kitu ambacho Rais huyo alikisema ambacho hakijulikani kwa umma. McMaster alimtetea Rais wake na kusema kulikuwa na mazungumzo ya mambo mengi katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi  Sergey Lavrov na Balozi wa Urusi Marekani Sergey Kislyak.

Gazeti la Washington Post lilieleza kuwa Trump aliwaeleza wageni wake hao jinsi ISIS wanavyotaka kutumia Laptop kama mabomu kwenye ndege,  aliongelea mambo mengine ambayo Marekani ilielezwa nanchi nyingine, na hili ndilo linaloleta kichwa kuuma kwani inaonekana Urusi wanaweza sasa kujua taarifa hizo zilitoka nchi gani. Tukikumbuka kuwa kuna uchunguzi unaoendelea kujua kama Urusi ilimsaidia Trump kushinda uchaguzi, wachunguzi wanaleta swali, Kwanini Trump anatoa taarifa za siri kwa Urusi na si kwa mataifa mengine rafiki? 
Wakati huohuo kura za maoni kuhusu utendaji wa Rais Donald Trump zinaonyesha hali mbaya kwa kiongozi huyo ambaye amekuwa  kazini kwa takriban siku 120 tu mpaka sasa. Kura za new Gallup tracking poll zilizotolewa Jumatatu hii zinaonyesha anaungwa mkono kwa  38% tu, ameshuka hata alipokuwa mwezi April. Kura hizi zinaungana na za  new NBC-Wall Street Journal poll zilizotolewa Jumapili zikionyesha utendaji wake wa kazi ukikubalika kwa  39%. Kura za Quinnipiac University poll zilizofanyika kabla Trump hajamfukuza kazi Mkurugenzi wa FBI James Comey, alionekana kukubalika kwa  36% tu. Na mwisho kura za Real Clear Politics average of all polls zinasema Trump anakubalika kwa  40.9%, na hakubaliki kwa 53.8%.Tamthilia ya Trump inaendelea

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.