USAILI WA KUJAZA NAFASI YA MKURUGENZI WA FBI WAANZA LEO


Rais Trump na James Comey

Usaili wa kujaza nafasi ya Mkurugenzi wa FBI umeanza. Nafasi hii imekuwa wazi baada ya Rais Donald Trump kumfukuza kazi mkurugenzi James Comey wiki iliyopita. Watu 11 wanategemea kusailiwa. Trump amejikuta akipingwa vikali kwa umamuzi wake wa kumfukuza Comey, ambaye alikuwa akiongoza upelelezi kuona kama Urusi ilihusika katika kuvuruga uchaguzi wa Marekani na kumuwezesha Trump kushinda uchaguzi huo, kuna wanaoona kuwa ni njama ya Trump kuvuruga upelelezi huo. Wakati huohuo kuna maswali yako hewani kujiuliza kwanini Rais Trump alimrekodi kisiri Mkurugenzi huyo wa FBI wakati wa mazungumzo yao ya kawaida. Habari hii imetokana na tweet aliyoiweka yeye mwenyewe Rais akionyesha kuwa kuna uwezekano kuwa yeye alimrekodi Comey. Jambo hili linatokana na maelezo ya Rais huyo katika barua yake ya kumfukuza kazi Comey kuwa Comey aliwahi kumwambia kuwa katika upeleleze unaoendelea kuhusu mkono wa Urusi katika uchaguzi, ‘Trump hayumo’. Sasa inasemekana Trump alirekodi hilo na mengineyo na sasa anamsubiri Comey akibadili tu maneno yeye atatoa kanda zenye mazungumzo hayo. Alipohojiwa na Fox news kuhusu hilo, Trump alisema hawezi kuongelea hilo, ila anamtaka Comey awe mkweli tu kila atakapohojiwa. Kiufupi, sinema hili la mahusiano ya Urusi katika uchaguzi wa Marekani bado bichiiiii

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.