VIMINI NA MINYWELE YA MARANGIRANGI MARUFUKU KWA WAALIMU WA KIKE


“Wanawake hawaruhusiwi kuvaa suruali kazini, isipokuwa kama ni kwenye michezo au akivaa suti kamili” Hayo ndio baadhi ya maneno katika waraka wa ndani kutoka idara ya elimu ya Manispa ya Hohoe, mkoa wa Volta huko Ghana. Katika waraka huo wanaume na wanawake walikumbushwa kuhusu uvaaji rasmi kazini-dress code.
Katika waraka huo uliochapishwa kwenye magazeti ya huko, waalimu waliambiwa kukwepa mini skirt na blauzi zisizo na mikono, wakwepe kujiremba sana na kutengeneza nywele za rangi mbalimbali. Wanaume waliambiwa wakwepe jeans na  T shirt zisizo na kola. Na waraka  ukaelezea kuwa kutakuwa na adhabu kwa watakaokiuka waraka huo. WaGhana wengi walionekana kukubaliana na waraka huo ambao una zaidi ya miaka 11 lakini ulikuwa haufuatwi na waalimu. Nchi mbalimbali duniani zilikuwa na kipengele cha kukataza akina mama kuvaa suruali kazini, Ufaransa iliondoa kipengele hicho mwaka 2013, sheria ya kuzuia wanawake kuvaa suruali Ufaransa ilipitishwa tarehe
 17 Novemba 1800. Shirika la ndege la Uingereza (British Airways lilianza kuruhusu wahudumu wa ndege zake wanawake kuvaa suruali  February 2016. Malawi ilikuwa na sheria ya kuzuia wanawake kuvaa suruali popote kuanzia mwaka 1965, na kuanza kuwaruhusu mwaka 1994. Uturuki, ilianza kuwa ruhusu wabunge wanawake kuvaa suruali Bungeni mwaka 2013, wakati Marekani ilianza kuruhusu Wabunge wake wanawake kuvaa suruali bungeni mwaka 1993. Sudan bado inawakamata wanawake wanaovaa suruali hadharani kupitia sheria yake na 152 ya makosa ya jina ya mwaka 1991.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.