VITA DHIDI YA UFISADI NIGERIA , KAMA SINEMA ZA NOLLYWOOD

VITA  dhidi ya ufisadi huko Nigeria imepamba moto, chombo kinachoratibu makosa ya rushwa nchini humo, the Economic and Financial Crimes Commission (EFCC), kimeieleza mahakama moja huko  Lagos kuwa mke wa mkuu wa usalama wa Taifa, aliyesimamishwa kazi hivi karibuni ndie aliyenunua nyumba ambamo fedha taslimu zaidi ya dola milioni 43 zikiwa na fedha nyingine za nchi mbalimbali zilikutwa. Kwa maelezo ya EFCC, mke wa Ayo Oke, Folashade Oke alitumia kampuni ya Chobe Ventures Limited kununua  Flat 7B, 13, Osborne Road ya Osbourne Towers, Ikoyi, Lagos. Na tarehe 13 April katika nyumba hiyo kulikutwa dola za Kimarekani milioni 43, pauni za kiingereza £27,800 na Naira za Kinaijeria milioni 23.2, zote zikiwa pesa taslimu. Kukamatwa kwa pesa hizi kulitokana na taarifa kutoka kwa wananchi. Nigeria imeanzisha taratibu ambapo anaetoa taarifa kuhusu ufisadi anagawiwa asilimia fulani ya fedha hizo. Kwa maelezo ya mwanasheria wa EFCC, Oke alinunua nyumba hiyo kwa kutoa kati ya August 25 and September 3, 2015 , alitumia jina la kampuni ya Chobe Ventures Limited kampuni ambayo ilikuja kugundulika haifanyi shughuli yoyote lakini Mrs Oke na mwanae Ayodele Oke Junior ndio wakurugenzi wa kampuni hiyo. Wakati huohuo EFCC imetaka fedha zilizokamatwa zitaifishwe kwani matangazo yaliyotolewa kupita magazeti kutanganza kupatikana kwa fedha hizo, hayaweza kumfanya mtu yoyote aje kudai kuwa fedha hizo ni zake. Kimsingi mamilioni ya dola hayana mwenyewe.  Rais  Muhammadu Buhari katikati ya mwezi April aliwasimamisha kazi kupisha uchunguzi, Babachir Lawal – Secretary General of the Federation (SGF) na Ambassador Ayo Oke – Mkurugenzi Mkuu wa National Intelligence Agency (NIA)  kutokana na wawili hawa kutajwa katika ufisadi. Uchungunzi huo unaongozwa na makamu Wa Rais wa nchi hiyo Yemi Osinbajo. Ayo Oke alisimamishwa kutokana na kupatikana kwa fedha zilizotajwa hapo juu wakati Babachir Lawal alituhumiwa kufisadi fedha zilizotakiwa ziende kwa wahanga wa Boko Haram.
Wakati huohuo tena  EFCC imesema imegundua zigo jingine la fedha, zinazodaiwa kutaka kutakatishwa. Fedha hizo kiasi cha Naira 448,850,000 zilikutwa kwenye duka moja katika LEGICO Shopping Plaza, iliyoko Ahmadu Bello Way, Victoria Island, Lagos. Fedha hizo zilizokuwa kwenye visalfeti inasemekana zilikuwa zinangoja kubadilishwa kuwa dola za Kimarekani. Mwezi Februari EFCC ilikuta dola milioni 9.8 na pauni  74, 000 fedha taslimu nyumbani kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Nigerian National Petroleum Corporation (NNPC), Andrew Yakubu.  Mheshimiwa huyo amedai fedha hizo alipewa zawadi na rafiki zake na ameenda mahakamani kupinga kitendo cha EFCC kumnyanganya mali yake.

1 comment:

Post Top Ad

Powered by Blogger.