WANAJESHI WAASI IVORY COAST WAFUNGA MITAA KUDAI BONASI


Jeshi la Ivory Coast limejipanga kuwakabiri askari wake waasi ambao wamekuwa wakifunga barabara na mitaa kwa siku ya tatu sasa.  Jiji la pili kwa ukubwa nchini humo Bouaké toka Jumamosi limo katika kadhia ya kufungwa kwa mitaa yake na wanajeshi wa nchi hiyo wanaotaka kulipwa bonasi. Waasi hao wameshasema kuwa wako tayari kupigana ikiwa wataaanza kuzuiwa kufanya fujo zao.
Wananchi kwa upande wao walianzisha maandamamno ya kupinga fujo za wanajeshi hawa, na wananchi 6 wamejeruhiwa baada ya kurushiwa risasi na waasi hawa.
Mkuu wa majeshi wa nchi hiyo General Sekou Toure alitangaza kuwa taratibu za kijeshi zinaandaliwa kumaliza vurugu hizo, japo wanajeshi wengine tayari waliaamua kufwata sheria na kuachana na uasi huo. Mwezi January wanajeshi waliilazimisha serikali kuwalipa bonasi ya zaidi ya shilingi 16,000,000/-
kwa kila askari, ilitegemewa kuwa malipo mengine yangefanyika mwezi huu, japo msemaji mmoja wa wanajeshi alitangaza kuwa wanajeshi wameamua kutokuchukua albaki hiyo na ndipo askari wengine wameingia mtaani wakidai hawakushirikishwa katika uamuzi huo. Serikali nayo kwa upande wake imesema haina mpango wowote wa kulipa fedhs nyingine. Kumekuwa na wasiwasi kuwa vurugu hizo zitalirudisha Taifa hilo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyochukua miaka 10 na kuisha 2011, maana waasi wengi walikuwa ni wale askari wapinzani waliojiunga na jeshi baada ya kwisha kwa vita.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.