WATUMISHI SITA WAFUKUZWA KAZI MANISPAA YA IRINGA

NA DENIS MLOWE, IRINGA
Madiwani  wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa

Toka kushoto, Mkurugenzi  wa Manispaa ya  Iringa  Dr Wiliam Mafwele anaefuata Mstahiki Meya Alex Kimbe

BARAZA la Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa limeridhia kufukuzwa kazi watumishi wake sita huku mmoja akirudishwa kazini.

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe akizungumza katika baraza la madiwani lilofanyika katika ukumbi wa Manispaa, alisema kuwa watumishi hao wamefukuzwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo utoro kazini kwa muda mrefu na suala la ulevi.

Kimbe alisema ndani ya Baraza hilo kuwa wamefukuzwa kazi kutokana na kutokuwepo kwenye vituo vyao vya kazi bila taarifa yoyote licha ya baadhi kuwa walikuwa na ruhusa ya masomo lakini hawakuweza kurudi mara baada ya muda wao wa masomo kwisha.

Alisema kuwa licha juhudi mbalimbali kufanyika katika kuwarekebisha na kuwapa onyo mbalimbali watumishi hao walishindwa kurudi kazini kwa wakati na wengine kuendelea na tabia ambazo hazitakiwa katika utumishi wa umma.
“Hawa watumishi sita wamefukuzwa kuanzia leo Mei 20, 2017. Hivyo Afisa Utumishi waandikie barua kuwapa taarifa hii" alisema.
Kimbe aliwataja watumishi waliofukuzwa katika halmashauri hiyo kuwa ni Anzawe Mvena, Glory Ngowi, Fransis Mkenge, Paul Sanga, Mkombozi Gendagenda na Tumaini Sanga
Alisema kuwa aliyekuwa mtumishi kwa upande wa mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wa Manispaa hiyo, Lucy Mtafya amerudishwa kazini baada ya kamati kuridhia makosa aliyotuhumiwa kufanya sio sahihi.
Alitoa wito kwa watumishi wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa uadilifu katika kuwaletea maendeleo wananchi na endapo mtumishi yoyote anataka kwenda kusoma lazima atoe taarifa.
Alisema ipo kasumba ya watu wapatato ruhusa ya kwenda kusoma au likizo wanakuwa hawarudi kwa wakati muafaka hali inayosababisha Manispaa kukosa baadhi ya wafanyakazi.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.