YANAYOENDELEA BAADA YA MAUAJI YA MANCHESTER, PICHA ZA MUUAJI ZAPATIKANA
 
HATIMAE picha za kwanza za Salman Abedi, kijana aliyejilipua na kuuwa watu 22waliokuwa wanatoka kwenye onyesho la muziki huko Manchester zimeanza kuenea mitandaoni. Na habari zaidi kuhusu kijana huyu zimeanza kupatikana. Wakati vyombo vya usalama vya Uingereza vinahangaika kujua mahusiano yake na makundi ya kigaidi, imejulikana kuwa Salman alikuwa kifanya safari za kwenda Libya mara kwa mara kutoka Uingereza. Salman alizaliwa Uingereza na wazazi wake wote ni wa kutoka Libya ambao walihamia Uingereza miaka mingi wakiwa wakimbizi wa utawala wa Kanali Gadafi. Rafiki yake mmoja wanae soma nae alisema, ‘Salman alienda Libya wiki tatu zilizopita na amerudi siku chache tu zilizopita.’
Salman alizaliwa Manchester, alilelewa katika jamii ya Libya ambayo ilikuwa na msimamo mkali wa kupinga utawala wa Kanali Muammar Gaddafi. Inasemekana wazazi wake walirudi Libya mara baada ya kuangushwa kwa utawala wa Gadafi mwaka 2011. Vyombo vya usalama vya Uingereza vinajaribu kuangalia itikadi za wazazi hao kwa wakati huu. Wakati huohuo polisi wa Uingereza wamesambazwa sehemu muhimu za nchi hiyo kama vile  Buckingham Palace, makao ya Malkia na Bungeni Westminster, na sehemu nyingine muhimu katika kujihami kama kutatokea shambulio jingine. Pia baada ya polisi kumkama mtu mmoja  jana Jumanne wameweza kuwatia nguvuni watu wengine watatu leo hii. Inadaiwa aliyekamatwa Jumanne ni kaka yake Salman

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.