ZIMBABWE HATARINI KUKATIWA UMEME


Kampuni ya kuzalisha umeme  ya Afrika ya Kusini Eskom, imesema itaikatia umeme Zimbabwe mwisho wa mwezi huu kama nchi hiyo haitalipa deni lake. Kitendo hicho kitaleta matatizo makubwa ya mgao nchini Zimbabwe na kuharibu uchumi wake ambao tayari una matatizo, japo ulitegemewa kupata nafuu mwaka huu kutokana na mazao mengi kupatikana nchini humo. Zimbabwe huagiza megawatt 300  kwa siku kutoka Eskom, mpaka sasa inadaiwa $44.5 millioni uhaba wa fedha za kigeni unalifanya taifa hilo lipate shida kubwa ya kulipa madeni yake. Kaimu Mtendaji Mkuu wa Eskom,  Matshela Koko amesema ZESA, ambalo ndilo shirika la umeme la Zimbabwe limekiuka makubaliano ya malipo, hivyo wao hawatakuwa na huruma kuhusu mpango wa kuikatia Zimbabwe umeme. Nae Mtendaji Mkuu wa ZESA
Josh Chifamba, alisema shirika lake linawasiliana na benki kuu ya Zimbabwe na hategemei kuwa kutakuweko na mgao. Mpaka Jumatatu hii Zimbabwe, ilikuwa inazalisha kwa siku Megawatt 1,051 MW, na Megawatt 350 zilikuwa zinaagizwa kutoka nje ya nchi. Matumizi ya nchi nzima ni Megawatt 1,500.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.