ASILIMIA 20 YA BAJETI ITATOKANA NA FEDHA WALIZOKAMATWA NAZO MAFISADI


Okoi Obono-Obla ambaye ni Msaidizi Mkuu wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amevieleza vyombo vya habari vya nchi hiyo kuwa asilimia 20 ya bajeti ya nchi hiyo, itatokana na fedha zilizokamatwa toka kwa mafisadi. Hii itafanywa baada ya kupitishwa na Bunge la huko.  Naibu Rais wa nchi hiyo Prof Yemi Osinbanjo ametia saini bajeti ya dola 23 bilioni, bajeti ambayo ni kubwa kuliko zote zilizowahi kutokea. Nigeria wameanzisha mtindo ambapo ukitoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ufisadi unapewa asilimia fulani ya fedha zitakazopatikana, mpaka sasa serikali imeshapewa taarifa ya matukio ya ufisadi 337, japo serikali bado haijataja kiwango kamili cha fedha zilizokwisha patikana

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.