BINTI WA RAIS ACHUNGUZWA KWA UTAKATISHAJI WA FEDHA

Binti wa Rais Denis Sassou Nguesso wa Kongo, Julienne Sassou Nguesso na mumewe  Guy Johnson wanapelelezwa na polisi wa Ufaransa kwa tuhuma za utakatishaji wa fedha na matumizi mabaya ya fedha za umma. Hii ni baada ya watu hao kununua nyumba ya dola 3.4 milioni katika eneo la watu matajiri katika jiji la Paris. Polisi wa nchi hiyo wanataka maelezo kujua fedha hizo zilitoka wapi. Si mara ya kwanza familia hii kujikuta kwenye vyombo vya habari kwa matumizi makubwa, mwezi Septemba mwaka 2006,  wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ujumbe wa Rais Sassou Nguesso ulikuwa pia na wanafamilia kadhaa ulikodi vyumba 44 vya hoteli ya gharama ya Waldorf Astoria kwa siku tano na kulipa jumla ya kiasi cha shilingi 299,000,000, fedha hiyo ilikuwa kubwa zaidi ya msaada uliotolewa na serikali ya Uingereza kwa nchi ya Kongo, kwa ajili ya huduma za binadamu kwa mwaka mzima wa 2006 !!!
Mwezi Julai 2007 shirika lisilo la kiserikali la Global Witness liliweka hadharani ripoti iliyoonyesha kuwa mtoto wa kiume wa Rais Nguesso, Denis Christel Sassou Nguesso, alitumia maelfu ya dola za Kimarekani zilizosemekana zilipatikana kutokana na mauzo ya mafuta ya nchi hiyo, kununua vitu mbalimbali jijini Paris. Katika ripoti hiyo ilisemekana katika mwezi wa Augosti 2006 peke yake kijana huyo alitumia dola 35,000 kunuua viwalo vyenye majina makubwa kama Louis Vuitton and Roberto Cavalli.
 Uchunguzi unaoendelea sasa pia unahusu matumizi ya wana familia wa marais watatu tofauti waCongo, Gabon na Equatorial Guinea, yanachunguzwa matumizi ambayo wameyafanya nchini Ufaransa


No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.