CONGO BRAZZAVILLE YAKOSA INTERNET KUANZIA IJUMAA ILIYOPITA


Nchi ya Congo Brazzaville haina internet ya uhakika kutoka Ijumaa 14, Juni 2017. Watoa huduma wa internet (Network Providers) wamesema tatizo linatokana na kukatika kwa waya (fiber optic), upitao chini ya maji katika bahari ya Atlantic Ocean, jirani na jiji la Pointe-Noire.
 Kampuni kubwa ya kutoa huduma za mawasiliano nchini humo, MTN Congo,  ilituma ujumbe wa sms kwa watumiaji wake wa internet siku ya Jumapili ikieleza kuwa kutakuwa na matatizo ya mtandao, na siku iliyofuata ikatuma ujumbe kuwa mtandao utakuwa unapatikana kwa shida. Cedric Nzimbou, mtaalamu wa wa mambo ya  mitandao anayefanya kazi katika kampuni ya  SkyTic Telecom, moja ya kampuni moja kubwa za huduma ya mitandao nchini humo alisema waya wa  fibre optic wa kilomita 12 ambao unaunganisha nchii hiyo na  West African Cable System (WACS) ulikatwa na meli mojawapo iliyokuwa inapita karibu na jiji la Pointe-Noire, hivyo kampuni yao ililazimika kutumia utaalamu wa V-SAT, ambao unatoa huduma ya internet lakini kwa spidi ndogo sana, hivyo kusababisha gharama ya matumizi kuwa kubwa. Tayari jopo la wataalamu walikwisha kwenda eneo la tukio kufanya matengenezo. Magazeti ya nchi hiyo yalikuwa yakilaumu meli za uvuvi za kichina kuwa ndizo zilizokata waya huo.
.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.