ETHIOPIA YAZIMA INTERNET KUZUIA WIZI WA MITIHANI


Ethiopia imekata mawasiliano yote ya internet nchini humo katika kile kilichoelezwa kuwa ni njia ya kuzuia wizi wa mitihani, katika wakati huu ambao kuna mitihani ya mwisho ya kitaifa ya darasa la Kumi. Ni mwaka wa pili mfululizo ambapo taratibu hizi zinachukuliwa na nchi hiyo. Report ya uwazi ya Google imesema kuwa mawasiliano kutoka nchi hiyo yalikatwa kutoka siku ya Jumanne.  Mwezi Juni mwaka 2016, maswali ya mitihani ya Kitaifa ya nchi hiyo yaliwekwa hadharani kwenye mitandao ya kijamii muda mfupi kabla ya mtihani na kuleta tatizo kubwa la kitaifa lililosababisha mitihani hiyo ifutwe, na kwa sababu hiyo nchi hiyo ikazuia mitandao ya Facebook, Twitter, Instagram and Viber. Miezi michache iliyopita Ethiopia ilifunga mitandao ya kijamii kutokana na kudaiwa kutumika kuhamasisha upinzani wa serikali katika mikoa ya Amhara na Oromia.
Mtindo wa kuzima internet unaonekana unanza kuenea Afrika kwani Uganda na Congo ziliwahi kuzima internet wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hizo. Cameroon iliwazimia Internet wakazi wa nchi hiyo walio katika maeneo yanayozungumza Kiingereza. Cameroon ina wazungumzaji wa Kiingereza na Kifaransa. Shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, mwaka jana lilitoa tamko kuwa kuwanyima watu matumizi ya internet ni kukiuka haki za binadamu.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.