GHOROFA LAPOROMOKA NA KUUWA WATU MJINI NAIROBI


Watu 15 hawajulikani waliko wakati watoto wawili wameokolewa wakiwa hai kutoka kwenye kifusi cha jengo la ghorofa saba ambalo limeporomoka katikati ya jiji la Nairobi masaa 24 baada ya jengo hilo kuporomoka.  Waokoaji kutoka Msalaba Mwekundu walisema watoto hao waliokolewa pamoja lakini pia ulipatikana mwili wa mwanamke mmoja.   Jengo lililoporomoka lilikuwa katika katika eneo linaloitwa  Pipeline Estate, lililoko kusini mwa jiji la Nairobi. Wiki moja kabla, jengo hilo lilipata nyufa na wakazi wake wakaziba nyufa hizo kwa simenti. Nyufa zika rudi tena Jumatatu asubuhi na ndipo majirani wakaitaarifu polisi na amri ya kuondoka kwenye jengo hilo ikatolewa, kiasi cha watu 128 walikubali amri ya kuondoka. David Kisia mmoja wa wakazi wa jengo hilo anasema alipigiwa simu akiwa kazini siku ya Jumamosi usiku kuwa jengo hilo limeporomoka, mpaka kufikia Jumanne mkewe na watoto wake watatu walikuwa bado hawajapatikana. Majengo mengi yaliyoko katika maeneo ya watu wenye kipato kidogo yanajulikana kuwa ni hatari kuishi lakini jitihada za kuyavunja zinashindikana kwani wentye nyumba hukimbilia mahakamani na kuweka pingamizi ya kubomolewa majengo hayo. Inasemekana sehemu lilipojengwa gharafa hilo ni sehemu ambayo haijapimwa na haijaruhusiwa kwa ujenzi , lakini wanasiasa wamekuwa wakilazimisha watu kupata nafasi ya kujenga majengo kama hayo na kuyapangisha. Polisi wanamtafuta mwenye ghorofa hilo ambaye ametambulika kwa jina moja tu la Karanja.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.