JENGO LA GHOROFA 24 LATEKETEA KWA MOTO LONDON


MOTO mkubwa umeteketeza kabisa jengo la ghorofa  24, huko London. Watu sita wameshatangazwa kuwa wamekufa katika moto huo, uliotokea kwenye jengo moja London Magharibi. Polisi wamesema kuna uwezekano mkubwa idadi  hiyo ikazidi. Mashahidi wanasema wakazi wa jengo, linaloitwa Grenfell Tower, walisikika wakiomba msaada wa kuokolewa au kuokulewa kwa watoto wao. Jengo hilo mpaka muda huu bado linaungua japo polisi walisema waliweza kuwaokoa watu wengi, Meya wa jiji la London alisema watu wengi hawajulikani waliko.  Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Theresa May ameelezea uchungu wake kutokana na jambo hilo. Zaidi ya askari wa Zimamoto 250 na ambulance 100 zilikuweko katika eneo hilo. Jambo la kushanganza ni kuwa jengo hili lilikuwa ndio kwanza limekamilika kufanyiwa ukarabati uliochukua maka miwili na kugharimu  £10m. Jengo hili lenye fleti 120, linamilikiwa na na Council ya Chelsea lakini linasimamiwa na  Kensington and Chelsea Tenant Management Organisation (KCTMO). Kabla na wakati wa ukarabati taasisi ya Grenfell Action Group iliwahi kutoa onyo kuwa jengo hili ni hatari kwa ajali za moto, kwani sehemu ya kupitisha magari wakati wa dharura ilikuwa ndogo sana. Tayari swala la kufanya uchunguzi wa kina kuhusu moto huu limeanza kudaiwa na wahanga wa ajali hii.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.