MAPOROMOKO YA ARDHI YAUA ZAIDI YA WATU 140

Kwa mujibu wa vyombo vya utangazaji vya serikali ya China, zaidi ya watu 140 inahofiwa wamezikwa katika tope baada ya maporomoko ta ardhi yaliyotokea jimbo la Sichuan, kusini magharibi mwa China. Pia kuna taarifa kuwa karibu kaya 40 zimeharibiwa kabisa katika kijiji cha Xinmo kwenye mkoa wa Maoxian. Waokoaji wanahangaika kujaribu kuokoa waliosalimika na kutoa miili iliyofukiwa chini ya mawe. Maporomoko hayo yametokana na mvua kubwa zilizonyesha katika jimbo hilo, na pia kutokana na eneo hilo kukosa miti, ilirahisisha maporomoko hayo. Maporomoko ya ardhi ni jambo ambalo si geni katika maeneo ya milimani huko China. Mwaka 2008 watu 87,000 walikufa maeneo hayohayo baada ya tetemeko la ardhi kusababisha maporomoka ya ardhi.


No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.