JE MGANDA KAFUNGUA KESI MWILI WA IVAN SSEMWANGA UFUKULIWE, FEDHA ALIZOZIKWA NAZO ZIONDOLEWE?


Inasemekana Mganda mmoja Abey Mgugu, leo hii 2-6-2017, amefungua shtaka katika Mahakama Kuu ya Uganda (Cause no. 196 of 2017), akiwataka  Bank of Uganda na kampuni ya mazishi ya  A-plus Funeral Services kufukua mwili wa  Ivan Ssemwanga na kuziondoa pesa zote alizozikwa nazo. Abey Mgugu amesema kuwa fedha zinazosadikiwa kuwa ni shilingi za Uganda, Rand za Afrika ya Kusini na Dola za Kimarekani lazima zifukuliwe katika kaburi hilo.

Anasema kufukia fedha zile katika kaburi ilikuwa ni matumizi mabaya ya mali ya umma, na hivyo kuingilia uhuru wa kijamii na kiuchumi wa watu wasiohusika. Hivyo alitaka fedha hizo zifukuliwe kwa niaba ya watu wa Uganda. A-plus Funeral Services ndio kampuni iliyoshughulikia mazishi ya Ivan Ssemwanga. Mgugu ameishtaki Benki Kuu ya Uganda kwa kosa la kwa uzembe au kwa makusudi kutokulinda heshima ya fedha za Uganda na za nchi nyingine. Siku Ivan Ssemwanga alipokuwa anazikwa wenzake wa kundi lilikuwa linajiita the rich gang walimwaga fedha kwenye kaburi kabla ya kuushusha mwili wa marehemu. Fedha hizo za noti za 10,000, 20,000 na 50,000 zilitupwa kaburini zikichanganywa na fedha za nchi nyingine hasa Marekani na Afrika ya Kusini.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.