MGODI WA NYAKAVANGALA KUFUNGWA KAMA WACHIMBAJI WATAENDELEA KUVUNJA SHERIA

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na juu ya kitu kinachoendelea kwenye mgodi wa Nyakavangala.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Wachimbaji  wanne katika mgodi wa Nyakavangala wamefukiwa na mchanga kutokana na wachimbaji hao kuingia kuchimba kinyume cha makubaliano yaliyowekwa baina ya wachimbaji na Mkuu wa Wilaya ya Iringa  Richard Kasesela.

Kasesela alisema kuwa siku ya tarehe 12 Juni, mida ya saa 1 jioni duara la mgodi mmoja ulioko Nyakavangala liliporomoka na kufukia wachimbaji 4 . 

"Inasemekana wachimbaji hao walikuwa wameingia kuiba kwani duara hilo ni kati ya maduara ambayo Mkuu Wa wilaya ya Iringa  Mhe Richard Kasesela aliifungia ili ijengwe nguzo na ngao" alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa watu wanne waliingia mgodini baada ya mafundi  wa ujenzi wa ngao kupumzika kwa vile ni usiku ndipo wachimbaji nao wakaingia mgodini bila ruhusa

"Hadi sasa tumefanikiwa kuokoa watatu, huyo mmoja hajaokolewa bado yupo ndani ya mgodi kutokana na changamoto za uokoaji ila juhudi zinaendelea za kumuokoa huyo mmoja" alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa changamoto ilikuwa ni namna ya kumuokoa kwani sehemu iliyokuwa imejifukia juu mwamba mwingine ulionekana kuwa na dalili za kushuka.ikawapasa kujengea kwanza eneo hilo kazi iliyochukua mda mrefu na ndipo waanze kumuokoa, kwa hiyo zinasubiri hatua nyingine sasa.

"Naendelea kuwaonya wachimbaji wasiendelee na uchimbaji eneo la chini maarufu kama kwenye "vein" mpaka wajenge ngao ili wasihatarishe maisha yao. Wakiendelea na kiburi tutaamua tufunge mgodi" alisema Kasesela

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.