MZEE WA KIHESA ALIYEKUWA NA ASILI YA KONGO, ALIYEZAA PILOT WA KWANZA KUTOKA KIHESA


MZEE MNYAWAMI KASONGO alikuwa ni moja ya wazee wa awali kabisa kuanza kuishi Kihesa. Mzee Kasongo ambaye asili yake ilikuwa ni mji wa Kisangani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, alianza kuishi Kihesa miaka ya 50. Mzee huyu alikuwa na wake wawili, ambapo mke wa kwanza alimzaa mtoto aliyeitwa Mwamba. Na hivyo kujulikana kama Mama Mwamba, mke wa pili wa mzee Kasongo aliitwa Binti Musa. Mwamba aliyekuwa mtoto pekee wa mzee huyu alifikia kuwa pilot wa ndege na bila shaka alikuwa pilot wa kwanza kutokea Kihesa. Ukoo huu ulizimika baada kufariki MzeeMnyawami, Mama Mwamba, Binti Musa na Mwamba mwenyewe. Mungu awalaze pemaNo comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.