SIMULIZI ZA WAZEE WA KIHESA - RUBEN NYALUSI


Mzee RUBEN NYALUSI alikuwa Mbena wa Lupembe, na alikuwa fundi stadi wa ujenzi na akaongoza umoja wa wajenzi Kihesa yeye akiwa mwenyekiti. Mzee huyu pia alijishughulisha na kilimo sehemu za Ngano Ismani, sambamba na Mzee Philipo Sawani. Hayati Mzee Nyalusi ndiye baba mzazi wa aliyekuwa mchezaji mahiri wa ile timu maarufu Kihesa Stars Simoni Nyalusi.
  Simon alikuwa mchezaji mmoja aliyekuwa na vituko vingi uwanjani, mpaka hivi leo kuna vituko alivyovifanya ambavyo waliokuweko hawataweza kuvisahau. Miongoni mwa vituko vya ajabu ni kitendo cha kupewa kadi nyekundu na refarii baada ya kumvuta pua mshika kibendera marehemu Bruda Modestus katika mechi kati ya Kihesa Stars na Lipuli, refa wa mechi hiyo Mzee Maselenge alimtoa nje. Kituko kingine ni siku akiwa mtazamaji kwenye mechi ya mashindano ya vyuo pale Kleruu aliingia uwanjani na kuifungia bao timu ya Kleruu na kusababisha mchezo kusimama takribani dakika 20 na wachezaji wa  timu ile ya Chuo cha Mbeya kuanza kumfukuza Simoni bila mafanikio yoyote.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.