ULISOMA SHABAHA AU HIGHLAND? UNAWAKUMBUKA HAWA? MWAL CHUNGU? MWAL SHEIKH?


Shule ya msingi ya Shabaha awali ilikuwa ikiitwa Aga Khan Primary School, ilikuwa jirani na shule ya Aga Khan Secondary School ambayo nayo sasa inaitwa Lugalo Secondary Secondary. Jina la Shabaha lilitokana na kuwa nyuma tu ya shule, pale mbele ya nyumba za Mzee Poyo, Mzee Makafu na Mtambule palikuwa na sehemu ambayo askari wa FFU walikuwa wakitumia katika kujifunza kulenga shabaha, watoto waliokuweko wakati huo watakumbuka kuwa mara baada ya mazoezi ya shabaha watoto walikuwa wakienda kuokota maganda ya risasi yaliyotumika. Moja ya waalimu wakuu wa kwanza wa Shule ya Msingi ya Shabaha  alikuwa Mwalimu Chungu, walimu wengine waliokuweko wakati huo walikuwa Mama Mbaruku ambaye ndiye alikuwa mwalimu wa darasa la kwanza, Mwalimu Kitojo akiwa mwalimu wa nidhamu. Jirani na shule hii ndipo ipo shule ya Highlands ambayo mwalimu mkuu wake wa kwanza alikuwa mwalim Sheikh, ambaye awali alikuwa mwalimu mkuu wa Aga Khan Secondary. Pale Highlands kulikuwa na walimu wengine kama mwalimu Chalamila, Mwalimu Mwambeta, Shawala, Mayagila, Mama Masima, Mwalimu Mpete na Mwalimu Mwakalinga. Listi hii ya waalimu ilikuwa ni listi tosha ya kuhakikisha akina Mohamed Siaga, Ally Sareva, Maneno Ndanzi na Robert Kipandule Nyato wanasoma ipasavyo.....una kumbukumbu za enzi zako shule yoyote ya Iringa? Tuma Picha au maelezo kwa whatsapp kwenye namba +255713274747 au kwa email jokitime@gmail.com  ili zitundikwe kwenye blog hii kwa furaha ya wote waliokuweko
 ASANDE

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.