WANAWAKE WAWABAKA WANAUME , POLISI WATOA TAHADHARI KWA WANAUME


POLISI  wa Zimbabwe wamewaonya wanaume wa jiji la Harare,  wawe na tahadhari kutokana na matukio mawili ambayo yalifikishwa kwenye vyombo vya dola hivi karibuni, ambapo wanaume walijikuta wakibakwa na wanawake baada ya kutoa au kupewa lifti. Msemaji wa polisi Chief Superintendent Paul Nyathi aliliambia gazeti la  The Herald, kuwa tukio la kwanza lilitokea jumapili jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 37 alipopanda basi na wanawake wawili. Anasema wakiwa njiani dereva wa basi aliwaambia anabadilisha njia ili kukwepa kizuizi cha polisi. Ghafla mmoja wa wanawake waliokuwa wameingia katika basi alitoa pisto na kumlazimisha mlalamikaji kuingia katika kichaka  pembeni ya barabara ya  Delport Road. Hapo ndipo mmoja wa wale wanawake alimlazimisha jamaa kufanya nae mapenzi wakati mwingine akamwesha kitu kilichomfanya azimie. Chief Superintendent Nyathi pia alielezea mkasa mwingine ambapo jamaa aliwapa lifti wanawake watano, njiani wakamkaribisha kinywaji, alipokunywa tu nae akazimia , alipopata fahamu akagundua kuwa akina mama wale wamemshughulisha bila ridhaa yake. Mwaka 2015 matukio haya yalikuwa mengi hasa ilipofika mwezi wa Septemba mwaka huo.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.