WAZEE MAARUFU WA KIHESA - PHILIPO SAWANIMzee huyu wa kabila la Kikinga ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Kihesa alikuwa mkulima eneo la Ngano Isimani, huku akiendesha biashara ya duka na bar hapo KIHESA katika nyumba yake ya kisasa kabisa. Wazee matajiri wa mji wa Iringa miaka hiyo kwa mfano Mzee Mwaitebele, Mzee Idd Mwangubi, Mzee Zabron Mwanyato pamoja na wafanya kazi maofisa kama Mzee Asam Sajio Kaduma walipenda kunywa kwenye bar ya Mzee Sawani. Lakini pia alipokuwa Mwenyekiti wa wilaya wa Tanganyika African Parents Association (TAPA) na alinunua jengo kwa pesa zake na kulifanya shule ya TAPA, shule ambayo kwa sasa inaitwa Shule ya Msingi Mtwivila. Na mwalimu wa shule hiyo wa kwanza alikuwa Mwalimu Edward Chaula ( Baba Kichupa ) na Joseph Msandi ambao mishahara yao ililipwa na mzee Philipo Sawani. Jully Sawani ni mtoto wa Mzee Sawani ambaye alikuwa diwani wa kwanza Kihesa. Mzee Sawani alikuwa  mtu nadhifu sana akipendelea kuvaa English suit. Ama kwa hakika Mzee Philipo Sawani ana mambo mengi sana aliyochangia kwa Kihesa na maisha ya wengi.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.