DC KASESELA ASULUHISHA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI


Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela tarehe 22/7/2017 allisuluhisha mgogoro wa wakulima na wafugaji katika kijiji cha Idodi, na kuamuru wale wote waliohusika kupiga wenzao wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Akizungumza na wazee na wafugaji wa jamii ya Kimasai na Kimang'ati pamoja na wakulima wa jamii ya Kihehe, alisisitiza suala la kutolisha mifugo kwenye mashamba ya watu na kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa. Mzee kutoka jamii ya Kimasai Mzee Bogati Six alimsifu lakini alilalamikia upendeleo unatolewa kwa jamii ya kifugaji ya Kimasai na kuwatenga Wamang'ati . Mkuu wa Wilaya aliamuru wafugaji wote walioko kwenye vyanzo vya maji waondoke mara moja.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.