MATAYARISHO YA VITA ENZI ZA MKWAWA

Kabla ya vita askari walivaa mavazi yao ya kivita, ngoma maalumu zikaanza kuchezwa. Mganga maalumu aliitwa na kutabili mwenendo wa vita. Askari walivuta bangi ili kupata mori unaotakiwa. Jeshi la Kihehe lilikuwa na vikosi vifuatavyo;
1.       Vatandisi- Wapelelezi. Hawa ndio walikuwa wakiwahi kujua kila habari kuhusu adui
2.       Kitengelemutwa- Bodyguards au walinzi maalumu wa Chifu
3.       Valambo – Kikosi cha mbele kilichomshtua adui (Shock troops). Inawezekana kuwa jina valambo lilitokana na neo lilambo ambalo maana yake ni bangi kwa Kihehe
4.       Valaya – Kikosi kilichofuatia Valambo
5.       Vanyambwe – kikosi kilichochakaza adui
6.       Vakanyilala – Kikosi kilichochakaza na kufanya adui kuwa daraja
7.       Vanyamwani – kikosi cha kutengeneza ngazi za kuparamia maboma au kuchoma moto
Kila kikosi kilikuwa na askari wapatao mia mbili.
Silaha zilizotumika zilikuwa;
1.       Lisala-  Mkuki mpana kwa kupigana ana kwa ana ulikuwa hautupwi, asikari alitumia kumchoma adui na kuchomoa na kutumia tena, tofauti na mikuki iliyokuwa miembamba ambayo alitupiwa adui
2.       Korofindo- Bunduki zilizokuwa zikipatikana toka kwa Waarabu
3.       Magobole- bunduki zilizotengenezwa na wafua chuma wenyeji

4.       Ngwembe – ngao ambazo zilitengenezwa kwa ngozi

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.