NYUMBA YA KATIBU WA UVCCM IRINGA MJINI YACHOMWA MOTO USIKU WA KUAMKIA LEO

Share:


Sehemu ya mali iliyoteketea

Mjumbe Wa Halmashauri kuu ya taifa Ccm Mnec Salim Asas akitoa salaam za pole

Mwathirika wa tukio akiwaonyesha viongozi wenzie, wanahabari, na wananchi  madhara aliyoyapata

Jana Jumanne kiasi cha saa tano usiku, kwa mujibu wa Alphonce Muyinga, alipokuwa amepumzika akasikia kioo cha chumba alichokuwa amelala kikivunjika na kitu kilitupwa ndani, baada ya hapo moto ukawaka. Moto huo umeunguza kila kitu kilichokuwa katika nyumba hiyo iliyopo maeneo ya Kihesa njiapanda ya Kwabeda . Kwa mujibu wa Kamanda wa zima moto James John, wao walipofika eneo hilo moto ulikuwa umeshika nyumba nzima hivyo walichojitahidi kufanya ni kuzuia moto usisambae nyumba za jirani, kamanda huyo amesema kutokana na maelezo ya Muyinga ambaye ni Katibu wa UVCCM Iringa mjini italazimika kuanza kufanya uchunguzi ili kujua waliohusika katika tukio hilo. Katibu Alphonce Muyinga anaamini kuwa kuchomewa nyumba huko ni kutokana na sababu za kisiasa

No comments