VICHEKESHO VYA KIHEHE

MDADA wa kazi toka Iringa alikuwa ndio kwanza kaanza kazi kwenye familia moja. Siku hiyo mume na mke wakwa wamealikwa kwenye sendoff ya binti wa rafiki yao. Wakawa wamemwambia yule segito kuwa wameenda sendoff. Wakati binti yuko peke yake akaja rafiki wa wenye nyumba ambaye bahati nzuri alikuwa Mhehe mazungumzo yakawa hivi;
MGENI Kamwene be
BINTI: Kamwene
MGENI: ndauli avanya kaye valikwi
BINTI: Vahele kwa Sendofu
MGENI: Vahele kwiya?
BINTI: Vatige vahele kwa Sendofu
MGENI: Kumbi Sendofu aikwikala kwi?
BINTI: Manye ne vandoje hele ukuta ene munu yoyote asile ndogage ukuta vahele kwa Sendofu. Mgeni akatoka anachekea tumboni


****************************************** 
 Mchina mmoja alijikuta pabaya baada ya kugongana na mama mmoja aliyekuwa amebeba kisado cha ulanzi, ulanzi ule ukamwagika. Mchina wa watu akajisikia vibaya akaanza kuomba msamaha,
MCHINA: I am velly soli, please I am soli
Kwanza akalambwa kibao, wakati amekunjwa sawasawa
SEGITO: Wi msenzi kabisa, ukwitulasi wa nene neke utige sole yinene?
MCHINA: I am soli velly soli.....(kipigo kikaendelea)


******************************************
Wakati wa enzi za ukoloni, viboko ilikuwa adhabu moja kubwa iliyotumika. Siku moja kijana mmoja wa Kihehe akakamatwa kwa wizi wa mahindi, alipopelekwa Bomani kwa hakimu mzungu akahukumiwa viboko vinne mara moja. Baada ya kutandikwa viboko vinne akaambiwa anaweza kwenda, aliposimama akamwambia mzungu, "Nyongise baba". mzungu akajua kijana kasikitika sana mpaka anaomba kuongezwa viboko. Akasema 'Ok unataka nikuongeze lala tena'. Viboko vinne vikatembea, kijana wa watu huku akilia akasema tena 'Nyongise' akaongezwa tena
*******************************************
Mamalaka inayoshughulika na mambo ya mvua imetoa taarifa kuhusu hali ya hewa kwa watu wa Dar es Salaam. Blog hii ilipomuuliza afisa mmoja ahatima ya mvua inayoendelea, alijibu kwa maneno mawili tu, 'Munia namwaka'. Mpaka sasa blog hii inajaribu kupepeleza alikuwa ana maana gani

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.